Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 25, 2023 Local time: 17:52

Nkunda: Hakuna Mgawanyiko Ndani ya CNDP


Kiongozi wa kundi la waasi wa CNDP wanao pigana na majeshi ya serikali mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amekanusha madai kuwa kuna mgawanyiko ndani ya kundi hilo.

Akiongea na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika leo (Jumatatu), Jenerali Laurent Nkunda amesema yeye bado ni kiongozi wa kundi hilo, na kwamba hakuna mtu ambaye anaweza kuleta mgawanyiko ndani ya kundi hilo.

Msemaji wa mkuu wa majeshi ya waasi, Jenerali Bosco Ntaganda, amekaririwa akisema kuwa makamanda walimfukuza jana Nkunda kutokana na uongozi mbaya. Lakini Nkunda amekanusha nakusema kuwa Ntaganda siyo msemaji wa CNDP au mwenyekiti.

Aidha Jenerali Nkunda amesema mazungumzo ya amani ya Nairobi yanaendelea vizuri licha ya vipingamizi vya hapa na pale.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG