Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 00:54

Gaza Yawaka Moto


Waziri wa ulinzi wa Israel amesema leo kuwa nchi yake iko katika vita kamili na kundi la wanamgambo wa Hamas, na ndege za kivita za Israel zimeshambulia vituo vya Hamas kwa siku ya tatu Ukanda wa Gaza.

Maofisa wa Israel wanasema mashambulio ya ndege za Israel yaliyoanza Jumamosi, yameuwa watu wasiopungua 315, wengi wao wanamgambo wa Hamas.

Kansela wa Ujeruman Angela Merkel amelaumu kundi la Hamas kwa ongezeko la machafuko kati yake na Israel. Hatahivyo ameiomba Israel kuepusha vifo vya raia katika mashambulio yake dhidi ya vituo vya Hamas.

Jana (Jumapili) katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon aliomba kusitishwa machafuko Gaza na kurejeshwa hali ya amani katika eneo hilo. Bwana Ban alisema analaani machafuko hayo na kwamba anasikitishwa na watu waliouwawa.

Aliomba pia Israel kufungua mpaka wake na Gaza kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia Gaza. Baraza la usalama la umoja huo limeomba pia kusitishwa kwa mapigano hayo baada ya saa kadhaa za mazungumzo ya dharura.

XS
SM
MD
LG