Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 20:27

Wanafunzi Wengi Washindwa Kufaulu Tanzania


Matokeo ya shule za msingi Tanzania yametoka na kuonyesha kuwa karibu nusu ya watahiniwa waliofanya mtihani wa kumaliza darasa la saba hawakuweza kupata alama zinazotakiwa kuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari.

Msemaji wa wizara ya elimu Tanzania, Mtandi Bunyanzu amesema leo kuwa watahiniwa 536,672 ambao ni sawa na asilimia 52.7 wamefaulu, wakiwemo wasichana 226,476. Hii inamaana kuwa karibu nusu ya wanafunzi wote waliofanya mtihani hawakuweza kufikia alama zinazotakiwa.

Matokeo haya yamekuja wakati serikali ya nchi hiyo ikiwa imeanzisha mpango wa kuendeleza elimu ya msingi na kukiwa na ongezeko kubwa la shule za msingi.

Lakini bwana Bunyazu anasema hii haina maana kuwa mpango huo wa kuendeleza elimu ya msingi umeshindwa, na kwamba hadhani kuwa ongezeko la shule za msingi zilizoanzishwa na watu binafsi linaweza kuwa limechangia wanafunzi wengi kushindwa kufaulu.

XS
SM
MD
LG