Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 04, 2023 Local time: 12:31

Wakimbizi Wakabiliwa na Hali Ngumu Kenya


Maelfu ya wakimbizi waliolazimishwa kuyakimbia makazi yao wakati wa machafuko yaliyofuatia uchaguzi wa rais nchini Kenya, wanakabiliwa na hali mbaya ya maisha, licha ya serikali ya nchi hiyo kuanzisha mpango wa kuwarudisha makwao.

Mmoja wa wakimbizi hao, Mase Wangui aliiambia Sauti ya Amerika kuwa hali ni mbaya katika makambi yao kiasi kwamba wanalazimika kujisaidia katika mifuko ya karatasi kutokana na kufurika kwa vyoo.

Wangui anasema hali hiyo imepelekea magonjwa ya aina mbalimbali na vifo katika makambi hayo, na kwamba kina mama wajawazito wanalazimika kujifungua katika mazingira magumu mno. Anasema hata kama msaada wa serikali utatolewa, huenda watu wengine zaidi watakuwa wamepoteza maisha.

Hali hiyo imepelekea mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kukosoa vikali mpango wa serikali ya Kenya wa kuwarudisha wakimbizi makwao au kuwapatia makazi mapya.

XS
SM
MD
LG