Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 22:57

Wanyarwanda Wafurahishwa na Hukumu Dhidi ya Kanali Bagosora


Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICTR imemhukumu kifungo cha maisha Kanali Theoneste Bagosora baada ya kumkuta na hatia ya mauaji ya maangamizi nchini Rwanda hapo mwaka 1994.

Mwandishi wa shirika la habari la mahakama hiyo ya Arusha Nicodemus Ikonko, anasema bado haijulikani Kanali Bagosora na maofisa wenzake wawili wa jeshi la zamani la Rwanda ambao pia wamehukumiwa vifungo vya maisha watatumikia wapi vifungo hivyo.

Uamzi huo wa mahakama ya kimataifa umepokelewa kwa furaha na kundi la watu walio nusurika na mauaji hayo- IBUKA- nchini Rwanda. Mwandishi wa Sauti ya Amerika aliyepo Kigali, Daniel Gakuba amemkariri Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo Benoit Kaboyi akisema hukumu hiyo itakuwa fundisho kwa wote wanaotumia madaraka waliyopewa vibaya.

XS
SM
MD
LG