Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 22, 2023 Local time: 18:35

Kagame: Simjui Jenerali Nkunda


Rais Paul Kagame wa Rwanda amekanusha madai kuwa nchi yake inahusika na machafuko yanayoendelea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kati ya serikali na waasi wa nchi hiyo wanaoongozwa na Jenerali Laurent Nkunda.

Mbali na kukanusha kuhusika na machafuko hayo, Rais Kagame anasema, "Sijawahi kamwe kuongea na Jenerali Nkunda, sijawahi kukutana na Jenerali Nkunda, na kwa kweli simjui mtu huyo zaidi ya kumuona kwenye televisheni."

Rais Kagame alichukua nafasi hiyo kuzikosoa serikali za magharibi ambazo anasema badala ya kuwajibika na makosa yao katika bara la Afrika, huwabebesha mzigo huo viongozi wa bara hilo na kukaa kimya pale wanapo husishwa na makosa hayo.

Licha ya Bwana Kagame na serikali yake kujaribu kujitenga na mapigano katika nchi jirani ya DRC, baadhi ya mataifa tayari yameanza kuchukua hatua dhidi ya Rwanda kufuatia ripoti iliyomo katika ripoti ya Umoja wa Mataifa inayoelezea mchango wa Rwanda katika machafuko ya DRC.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa inaihusisha Rwanda na kikundi cha waasi wa CNDP nchini DRC kinachoongozwa na Jenerali Nkunda.

XS
SM
MD
LG