Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 08:49

Familia ya Obama White House


Ikulu ya Marekani, White House inajiandaa kwa familia mpya ya rais mteule, Barack Obama ambayo inatazamiwa kuhamia hapo wiki chache zijazo. Bwana Obama, mkewe na watoto wao wakike wawili, watapata makao mapya na kuanza maisha mapya katika jumba la kifahari na maarufu duniani.

Kuingia kwao katika jumba hilo yatakuwa mabadiliko makubwa kwa nchi nzima na kwa familia hiyo. Barack Obama, Michelle Obama na watoto wao wawili wataondoka nyumba yao ya ghorofa tatu mjini Chicago na kuingia katika jumba la kale la miaka 200.

Jumba hilo lina vyumba vya kihistoria vya serikali, na ghorofa ya pili ambayo haionyeshwi sana kwa umma, ndio yatakuwa makao yao.

Kuna wafanyakazi 80, lakini Michelle Obama anasema ameshawaambia wafanyakazi hao kuwa wasichana wao Malia na Sasha watapaswa kujitandikia vitanda vyao wenyewe na kuviweka vyumba vyao katika hali ya juu ya usafi bila msaada wowote.

XS
SM
MD
LG