Watu wengi duniani
wanachukulia hii leo kwamba kuwepo na haki za binadam ni chombo muhimu cha
jamii iliyostarabika. Lakini larry cox wa Amnesty International, AI kitengo cha Marekani anasema mkataba wa haki za binadam ni matokeo ya wakati muhimu kabisa
ya historia duniani.
Umoja wa Matiafa hatimae ukapitisha mkataba kwa kura 48 bila ya kupingwa, na ikabidi kuchukuliwe hatua kubwa za kidiplomasia kuyarai mataifa mengine duniani kukubaliana na mkataba huo.
Bi Mariam Kahiga mkurugenzi
wa AI huko Kenya anasema mkataba huo umeleta manufaa chungu nzima kwa Afrika. Anasema jambo moja kuu ni kuyasaidia mataifa kupanga na kupitisha sheria za kitaifa za haki za binadam