Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 23:39

Miaka 47 ya Uhuru wa Tanganyika


Watanzania waadhimisha miaka 47 ya uhuru huku wakiwa na wasi wasi kwamba maadui watatu walotajwa na baba wa taifa marhemu Mwalimu Julius Nyerere alipotangaza uhuru, ujinga, ugonjwa na umaskini hawajashindwa baado.

Wachambuzi na raia walozungumza siku ya Uhuru tarehe 9 Disemba, wanasema miaka inapoendelea maadui hao watatu wamezidi kua sugu huku vita dhidi yao ikipunguka.

Akizungumza na Sauti ya Amerika kiongozi wa chama cha upinzani cha wananchi CUF profesa Ibrahim Lipumba anasema licha ya mafanikio kadha ya kisiasa yaliyopatikana katika uhuru Tanzania bado inakabiliwa na changamoto ya kukabiliana na umaskini.

Lipumba anasema kufuatanba na takwimu za serekali, kati ya mwaka 2001 hadi 2007 umaskini wa kutupwa nchini Tanzania umeongezeka kwa kuongezeka watu milioni mbili zaidi, hiyo ikimanisha anasema asili mia 30 ya wa-Tanzania wanaishi katika ufukara kabisa.

Tanganyika ilijinyakulia uhuru kutoka kwa ukoloni wa Uingereza mwaka 1961 na kungana na Zanzibar mwaka 1964 kuunda Jamhuri ya Mungano ya Tanzania.

XS
SM
MD
LG