Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 12:47

Vyombo vya Habari Kubanwa Kenya


Bunge la Kenya limeahirisha mjadala juu ya mswada wenye utata wa kuviwekea udhibiti mkali vyombo vya habari vya nchi hiyo.

Mwandishi wa habari wa gazeti la Daily Nation la Kenya, Douglas Mutua ameiambia Sauti ya Amerika kuwa hii ni moja kati ya mbinu nyingi za serikali na bunge kunyamazisha waandishi wa habari ambao wamekuwa wakishinikiza viongozi hao walipe ushuru kama wananchi wengine wa kawaida.

Bwana Mutua anasema mswada huo unatoa mamlaka kupita kiasi kwa waziri wa habari kiasi kwamba atakuwa na uwezo wa kuvamia na kufunga kituo chochote cha habari kwa madai kuwa kituo hicho hakizingatii maadili ya vyombo vya habari.

Chini ya mswada huo, Mutua anasema, wamiliki wa vyombo vya habari watatakiwa kuwa na kituo cha televisheni, radio na magazeri. Anasema waandishi wa habari wa Kenya hawako tayari kunyamazishwa na wanasiasa wanao jaribu kutumia mswada huo kuzuwia sauti za wananchi.

XS
SM
MD
LG