Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 07:50

Blair: Kunaweza Kuwa na Taifa Moja la Palestina


Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza, Tony Blair amesema mashauriano ya amani kati ya Israel na wapalestina hayatafanikiwa mpaka hali halisi iboreke huko kwa pande zote.

Akiongea hapa Washington, bwana Blair alisema lazima kuboresha pande zote kabla ya makubaliano yoyote kuwezekana.

Amesema, "Tatizo ni kwamba mpaka hivi sasa ukweli ni kwamba waisrael na wapalestina hawajapitisha kile ambacho naweza kukiita ni maelewano ya kawaida katika kusogeza mbele mashauriano ya amani ili yafanikiwe."

Bwana Blair ambaye amekuwa mwakilishi wa umoja huo kwa muda wa miezi 18 iliyopita, anasema hivi karibuni kumekuwepo na maendeleo kidogo huko ukingo wa magharibi. Anasema majeshi ya usalama ya Palestina yamefanikiwa kupelekwa katika miji ya ukingo wa magharibi ya Jenin, Nablus na Hebron.

XS
SM
MD
LG