Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 07:07

Mamia Wauwawa Nigeria
Wanajeshi wa Nigeria wanafanya doria katika mji wa Jos baada ya mamia ya watu kuuwawa wakati wa machafuko ya siku mbili kati ya waislam na wakrito.

Hali katika mji huo ilikuwa tulivu jana baada ya majeshi ya nchi hiyo kuweka amri ya kutotoka nje katika baadhi ya maeneo ya mji huo. Maofisa wa Nigeria wanasema polisi wamekamata mamia ya watu wanaodhaniwa kuhusika na mapigano hayo.

Msikiti mkubwa katika mji wa Jos unaripoti kuwa ulipokea miili ya watu wasiopungua 350 waliouwawa katika machafuko hayo, wengi wao walizikwa haraka na ndugu zao.

Haijulikani ni watu wangapi ambao siyo waislam waliuwawa katika mji wa Jos ambao ni mji mkuu wa Plateau nchini Nigeria.

XS
SM
MD
LG