Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 14, 2024 Local time: 23:28

Mashitaka ya Rushwa Tanzania


Mahakama kuu ya Tanzania imesema washitakiwa Daniel Yona aliyewahi kuwa waziri wa nishati na madini, na Basil Mramba aliyewahi kuwa waziri wa fedha, wanahaki ya kuweka dhamana ya mali isiyohamishika yenye thamani ya shilingi bilioni mbili nukta saba kila mmoja.

Uamuzi huo wa mahakama kuu unatengua ule uliokuwa umetolewa na mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, uliotaka washitakiwa kuweka dhamana ya shilingi bilioni tatu nukta saba kila mmoja.

Hadi leo jioni viongozi hao waandamizi wa serikali ya awamu ya tatu na ya nne walikuwa katika harakati za kukamilisha masharti hayo ya dhamana yaliyotolewa na mahakama kuu.

Wakati huo huo, dokta Semboja Khaji Khatibu wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, amesema hatua hiyo ya serikali kuwakamata na hatimaye kuwafikisha mahakama vigogo hao wazamani katika serikali ya nchi hiyo imerejesha imani ya wananchi wa kawaida kwa serikali ya nchi hiyo.

XS
SM
MD
LG