Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 13:25

Wakenya Wasubiri Mabadiliko ya Baraza la Mawaziri


Wakenya wanawasubiri rais Mwai Kibaki na waziri mkuu Raila Odinga kufanya mabadiliko katika baraza la mawaziri. Asilimia 80 ya wakenya wanakabiliwa na hali mbaya ya maisha kutokana na kupanda kwa bei za vyakula, na wengi wao wanataka serikali kumteuwa waziri wa fedha kuwaongoza katika masuala ya fedha na uchumi.

Wizara hiyo nyeti ya fedha ilibaki wazi baada ya aliyekuwa waziri katika wizara hiyo Amos Kimunya kujiondoa kuruhusu uchunguzi wa uuzaji hoteli ya kifahari ya Grand Regency kufanyika. Katika kashfa hiyo, inadaiwa kuwa waziri huyo wa zamani alitumia vibaya mamlaka yake na kwa kulikuwa na vitendo vya ufisadi. Waziri huyo alikanusha kuhusika na ufisadi wowote.

Hivi karibuni rais Kibaki alimteuwa mwanasiasa mkongwe John Michuki kuchukua wadhifa huo, lakini bwana Michuki akakataa. Wiki hii Jaji mkuu Majid Cocker alimkabidhi rais Kibaki ripoti ya uchunguzi uliofanywa kuhusu mauzo ya hotel hiyo kwa serikali ya Libya.

XS
SM
MD
LG