Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 04:09

Obama na Uchumi


Rais mteule wa Marekani Barack Obama ameweka wazi kuwa uchumi wa Marekani unao chechemea utapewa kipaumbele zaidi akiingia madarakani Januari 20.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika Jim Malone anaripoti kuwa Bwana Obama amefanya mikutano na waandishi wa habari siku tatu mfululizo kutangaza watu wanaounda timu yake ya uchumi, na kuwahakikishia wananchi kuwa suala la kuinua uchumi liko juu kwenye ajenda yake ya uchumi.

Bwana Obama amesema, "Kipaumbele na kazi yangu ya kwanza ni kuweka uchumi katika hali bora zaidi, kuunda nafasi milioni mbili na nusu za kazi na kutoa ahueni kwa familia za watu wa daraja la kati."

Wapiga kura walisema uchumi dhaifu wa Marekani lilikuwa suala muhimu katika uchaguzi wa rais, na kwa sababu hiyo bwana Obama hana njia nyingine, bali kutoa kipaumbele zaidi kwa uchumi hata kabla ya kuapishwa kwake kama rais Januari 20.

XS
SM
MD
LG