Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 24, 2023 Local time: 17:36

DRC Yashutumiwa kwa Mauwaji


Shirika la kutetea haki za binadamu linasema majeshi ya serikali ya DRC yameuwa watu wapatao 500 waliodhaniwa kuwa wapinzani wa serikali, ripoti ambayo imeungwa mkono na mtetezi wa haki za binadamu nchini humo Alexis Kanyenye.

Kwa mujibu wa Kanyenye, pande zote husika katika mgogoro wa nchi hiyo, majeshi ya serikali na waasi wa CNDP wanaoongozwa na Jenerali Laurent Nkunda, wamekuwa wakiuwa raia wasiokuwa na hatia.

Amesema majeshi ya serikali yamehusika zaidi na uporaji mali, huku waasi wa CNDP wakienda nyumba kwa nyumba na kuuwa vijana wenye umri wa miaka kuanzia 15, wakiwashutumu kuunga mkono wana mgambo wa Maimai.

Bwana Kanyenye amesema shirika lake na makundi mengine ya kutetea haki za binadamu waliwaandikia barua mara kadhaa waasi wa CNDP na serikali kuwataarifu kuhusu vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu, na kwamba wanaushahidi wa kutosha kuweza kuwafungulia mashitaka watu wanaodhaniwa kuhusika na mauwaji hayo.

XS
SM
MD
LG