Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 25, 2024 Local time: 16:42

Odinga: Majeshi ya Kulinda Amani Yapelekwe Zimbabwe


Waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga amewaomba viongozi wa Afrika kumzuwia rais Robert Mugabe kuhudhuria mikutano ya muungano wa Afrika hadi pale suluhisho la kisiasa litakapo kuwa limepatikana nchini Zimbabwe.

Wito huo wa bwana Odinga umekuja wakati viongozi mashuhuri wa Afrika wakiwa wameanza juhudi mpya za kujaribu kuleta maridhiano kati ya rais Mugabe na kiongozi wa chama cha upinzani Movement for Democratic Change bwana Morgan Tsvangirai.

Bwana Odinga amesema wakati umewadia kwa viongozi wa Umoja wa Afrika kumchukulia hatua kali rais Mugabe kwa kukaidi makubaliano ya kuunda serikali ya mseto ya nchi hiyo.

Kufuatia mvutano unaoendelea kati ya upinzani na serikali ya chama tawala cha ZANU-PF, bwana Odinga amesema, "Nafikiri wakati umewadia kwa nchi za Afrika kusimama kidete kutetea demokrasia nchini Zimbabwe" na kuongeza kuwa, "Kwa kuwa hakuna serikali halali nchini Zimbabwe, Umoja wa Afrika inabidi ufikirie kupeleka jeshi la kulinda amani nchini Zimbabwe."

XS
SM
MD
LG