Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 14:54

Uhusiano wa Russia, Marekani Chini ya Obama


Rais mteule wa Marekani Barack Obama atakabiliwa na masuala kadhaa ya ndani na yakimataifa baada ya kuapishwa Januari 20, ikiwemo sera ya Marekani inayotakiwa kufuatwa dhidi ya Russia.

Wachambuzi wengi wanakubaliana kuwa uhusiano kati ya Washington na Moscow siyo mzuri, na baadhi ya wataalam wanasema wazi kuwa ni mbaya. Marshall Goldman wa chuo kikuu cha Harvard mjini Washington, anasema pande zote mbili zimechangia kuzorota kwa uhusiano huo.

Bwana Goldman anasema, "Marekani chini ya rais George W. Bush ilifuata sera ambayo wa-Russia waliichukulia kama ya upande mmoja katika juhudi za kudhoofisha nafasi ya Russia katika mfumo wa siasa wa dunia."

Wakati huo huo, Goldman anasema wa-Russia walifanya mambo, hususan vita ya Georgia, ambayo yaliwakasilisha wamarekani na viongozi wa Marekani. Anasema miaka michache iliyopita wakati uchumi wa Russia ulipokua kutokana na bei kubwa ya mafuta, Moscow ilitaka kurejesha nafasi yake kama taifa lenye nguvu zaidi kimataifa.

XS
SM
MD
LG