Wakati huo huo waasi kutoka kundi la Laurent Nkunda wamesonga mbele na kufikia kilomita 20 za mji wa Kanyabayonga, kilomita 90 kaskazini ya Goma. Nkunda anasema majeshi yake yatasimamisha mapigano kuruhusu majeshi ya walinda amani wa umoja mataifa MONUC kuingia katika eneo hilo.
Ufaransa imewasilisha pendekezo la kuongeza idadi ya walinda amani kwa wanajeshi elfu tatu, pendekezo linalotarajiwa kuidhinishwa baadae wiki hii. Ofisi ya MONUC yenye karibu watu elfu 17 huko DRC ina walinda amani elfu 5 katikia jimbo la Kivu ya kaskazini.
Na iliripotiwa kwamba majeshi ya serekali yaliyokua yakikimbia kutoka Kanyabayongo yalipambana na wanamgambo wa Mai Mai, ambao kawaida ni washirika wa serekali. lakini mkuu wa kijiji cha Kirumba Ladislas Kasira Kambala anasema wanajeshi wa serekali walikua wakipora mali ya wananchi na wapiganaji wa Mai Mai katika eneo walijaribu kuwazuia huku wananchi wakilazimika kukimbia alfajiri Jumanne.