Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 11:09

Rwanda yadai kuachiliwa mshauri wa Kagame


Vijana huko Rwanda wamendelea na maandamano kote nchini kulalamika dhidi ya kukamatwa kwa mkurugenzi mkuu wa itifaki katika afisi ya rais, Bi Rose Kabuye, ambae pia ni mshauri wa Rais Paul Kagame. Wandalizi wa mandamano hayo vijana wa mji wa Kigali na majimbo yote ya Rwanda waliandamana hadi ubalozi wa Ujerumani na kudai kwamba wataendelea kuandamana hadi kuachiliwa huru Bi Kabuye. Rais Kagame, hakuahirisha ziara yake ya kikazi huko Ujerumani na alimtembelea mshauri wake huko jela.

XS
SM
MD
LG