Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 11, 2023 Local time: 04:02

Miriam Makeba Aaga Dunia


Ni siku ya huzuni kwa bara zima la afrika na ulimwengu kwa ujumla, kwani Miriam Makeba ambae jina lake la kuzaliwa ni Zenzile Makeba alifariki akifanya kile alichokua akipenda kufanya miaka yote, nayo ni kuimba. Taarifa ya familia yake inaeleza kwamba Makeba alianguka baada ya kuimba nyimbo yake mashuhuri pata pata na kupata mshtuko wa moyo.

Mjuku wake Nelson Lumumba Lee alikua pamoja nae na rafiki yake wa muda mrefu, promote wa kitaliana Roberto. Nyimbo za Makeba zilipigwa marufuku Afrika Kusini kwa zaidi ya miaka 30 wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi. Akalazimika kuishi uhamishoni wakati wote huo hasa huko afrika magharibi nchini Guinea, Conakry. Aliimba pamoja na waimbaji mashuhuri duniani ikiwa ni poamoja na Nina Simone, Dizzy Gillespie, Harry Belafonte na Paul Simon.

Nyimbo yake iliyowavutia wengi ni ile ya "click song" na "malaika". Lakini nyimbo ya kuonesha uzalendo na vita vyake dhidi ya ubaguzi wa rangi ni sophiatown.

Mwaka 1955 serekali iliwahamisha kwa nguvu watu elfu 60 kutoka kitongoji cha Sopiatown na kuwajengea makaburi maskini nyumba za mapato ya chini na kuupatia mji jina la Triomf.

Mwaka 1990 Makeba akaombwa na rais wa zamani wa Afrika Kusini kurudi nyumbani. Hakupendelea mwanzoni maana alidhani waafrika kusini wenzake hawapendi tena muziki wake, lakini kinyume na hicho alipendwa sana. Na Mandela akitowa heshima zake alimueleza kama mama wa kwanza wa nyimbo na mama wa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi. Miriam Makeba alifariki akiwa na umri wa 76 aliza mtoto mmoja tu Bongi aliyefariki 1985.
XS
SM
MD
LG