Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 00:15

Nchi za Afrika Kupeleka Majeshi DRC


Kufuatia kuongezeka kwa mapigano na mauwaji ya raia katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baadhi ya nchi za Afrika zimesema kuwa ziko tayari kupeleka majeshi yake nchini humo kusimamisha mapigano hayo.

Hatua hiyo inafuatia mapigano ya siku kadhaa kati ya majeshi ya serikali na waasi wa CNDP wanaoongozwa na Jenerali Muasi Laurent Nkunda. Katika mapigano hayo idadi isiyojulikana ya raia wameuwawa na maelfu kwa maelfu kulazimika kuyakimbia makazi yao.

Katika mahojiano na Sauti ya Amerika leo, msemaji wa waasi Bertrant Bisimwa amesema wanataarifa kuwa nchi za SADC ikiwemo Angola, wanajiandaa kupeleka majeshi yao nchini DRC kusaidia jeshi la serikali katika vita hiyo.

Bwana Bisimwa amelaani hatua hiyo kwa maelezo kuwa majeshi hayo ya kulinda amani yatakuwa yanaegemea upande mmoja wa serikali kwa kupambana na waasi wa nchi hiyo. Anasema Vita ya Congo ni tatizo la Congo, na kwamba tatizo hilo litatatuliwa na wa-Congo wenyewe.

Kiongozi wa waasi hao Jenerali Laurent Nkunda amekaririwa akisema kuwa wapiganaji wake watashambulia majeshi ya kulinda amani kutoka Afrika kama yakipelekwa nchini humo kusaidia serikali.

Wakati huo huo, kunataarifa za mauwaji ya raia wasiokuwa na hatia hususan vijana ambayo yanadhaniwa kufanywa na waasi. Lakini madai hayo yamekanushwa na msemaji wa waasi bwana Bisimwa, ambaye anasema waliingia katika mtego wa serikali ambayo inatafuta kuungwa mkono na mataifa mengine ya Afrika katika vita hiyo.

Waasi wa kitusi wamekuwa wakipigana na majeshi ya serikali DRC kwa madai kuwa wanajaribu kulinda maslahi ya watusi nchini humo.

XS
SM
MD
LG