Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 09:45

Uchaguzi wa Baraza la Wawakilishi Marekani


Ushindi katika chaguzi nyingine za ubunge Marekani umekipa chama cha Democratic na spika wa bunge Nancy Pelosi, ongezeko la wingi katika baraza la wawakilishi.

Wakifaidika na wimbi lililofanikisha kuchaguliwa kwa seneta Barack Obama kuwa rais, wa-Democrat wanaelekea kushinda viti 260 au zaidi katika baraza la wawakilishi.

Ukikusanya viti vilivyo chukuliwa katika seneti, na kuwafanya wakaribie wingi wa viti 60, wa-Democrat wataanza bunge jipya la 111 mwezi Januari wakiwa na nguvu kubwa kuliko wakati wowote ule tangu mwanzoni mwa miaka ya 1990, huku wa-Republican watakuwa na viti 175.

Kwa rais mteule Obama ambaye alihimiza enzi mpya ya umoja katika hotuba yake huko Chicago Jumanne usiku, mgawanyo wa bunge unampa uwezekano wa kazi rahisi kupitisha ajenda zake bungeni.

Spika wa bunge Nancy Pelosi alisema wa-Democratic wapo tayari kufanya kazi na Obama na kufanya kazi kwa ushirikiano mpya.

Spika Pelosi alisema lazima wachukue tahadhali sana kwa uthabiti wa Marekani, na kwamba hilo ndio hasa rais mteule Obama anajiandaa kufanya kama rais ajaye wa Marekani.

Seneta Chuck Schumer alizungumzia nguvu ya pamoja kwa wa-Democrat akisema, siku za wa-Republican kuzuwia mambo zimekwisha, na kwamba wa-Democrat katika seneti na wenzao katika baraza la wawakilishi, watafanya kazi pamoja kuirudisha Marekani kwenye mtizamo sawa baada ya miaka nane.

XS
SM
MD
LG