Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 23:48

McCain, Obama Walenga Zaidi Majimbo Muhimu


Mgombea urais Marekani wa chama cha Democratic Barack Obama na mpinzani wake John McCain wa Republican wanaanza siku ya leo Pennsylvania, katika kugombania majimbo muhimu wiki moja kabla ya siku ya uchaguzi.

Seneta Obama atafanya kampeni katika miji ya Chester, Pennsylvania na Virginia ya Harrisonburg na Norforlk, kwa matumaini ya kupata kura muhimu katika majimbo hayo.

Kwa kawaida Virginia huchukuliwa na warepublican, lakini maoni yanaonyesha kuwa Obama huenda akashinda jimbo hilo Novemba nne.

Seneta McCain anatembelea miji ya Harrisburg na Allentown katika jimbo la Pennsylvania, kabla ya kuelekea kusini kufanya kampeni katika mji wa kijeshi wa Fayettevelle katika jimbo la North Carolina.

XS
SM
MD
LG