Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 21:00

Obama Asitisha Kampeni


Mgombea urais wa chama cha Democratic Barack Obama atasitisha kampeni yake baadaye wiki hii kumuuguza bibi yake ambaye hali yake imeripotiwa kuwa mbaya sana.

Maofisa wa kampeni walisema jana kuwa Obma atasitisha shughuli nyingi za kampeni kwa siku ya Alhamis na Ijumaa ili kumuuguza Madelyn Dunham mwenye umri wa miaka 86 na ambaye alisaidia sana kumlea Obama.

Maofisa hao walisema hali ya Dunham imezidi kudhoofika kiasi kwamba imekuwa mbaya mno. Mapema jana Obama na mpinzani wake John McCain wa chama cha Republican waliwaendea wapiga kura katika majimbo muhimu, wakati kampeni zao zikiingia wiki mbili za mwisho kuelekea uchaguzi mkuu.

Kura za moni zinaonyesha kuwa Obama anaongo, lakini zikiwa zimebaki wiki mbili kabla ya uchaguzi kufanyika, matokeo hayo yanaweza kubadilika.

XS
SM
MD
LG