Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 11:41

Colin Powell Amuunga Mkono Obama


Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani Colin Powell amemuunga mkono mgombea urais wa chama cha Democratic Barack Obama, wiki mbili kabla ya wamarekani kumchagua rais wao.

Akiongea jana na kituo cha Televisheni cha NBC news, jenerali Powell alisema Obama ameonyesha kuwa yuko tayari kukabiliana na changamoto kubwa zinazo likabili taifa hili.

Alisema uamuzi huo haukuwa rahisi kwani amekuwa rafiki wa karibu na mgombea urais wa chama cha republican, lakini pia anasema kwa kipindi cha miaka miwili ambacho amekuwa akifuatilia kampeni ya Obama, ameridhika kuwa yuko tayari kulipeleka taifa hili katika mwelekeo unao faa.

Alipo ulizwa kama kama hatua yake ya kumuunga mkono Obama itasaidia katika uchaguzi huu na hasa ikizingatiwa kuwa aliunga mkono vita ya Iraq, jenerali Powell alisema yuko pale kutoa maoni yake kuhusu nani anadhani kuwa anasera nzuri ya kuliinua taifa hilo, na siyo kuwalazimisha wamarekani kuhusu mtu wa kumpigia kura.

Jenerali Powell alikuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani katika utawala wa rais George W. Bush, na aliongoza vikosi vya kimataifa wakati wa vita ya kumuondoa Sadam Hussein kutoka Kuweiti.

XS
SM
MD
LG