Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 28, 2025 Local time: 19:04

Papa Francis alipata nafuu leo Jumanne baada ya kutaabika na homa ya mapafu


Papa Francisco akiwa Vatican katika picha iliyochukuliwa Februari 5, 2025.
Papa Francisco akiwa Vatican katika picha iliyochukuliwa Februari 5, 2025.

Papa Francis alipata nafuu mapema Jumanne baada ya kutaabika katika mapambano yake dhidi ya homa ya mapafu yake, matatizo mawili mapya ya kupumua ambayo yalimlazimu kuanza tena kutumia mrija wa uingizaji hewa kwa ajili ya kupumua. Katika taarifa yake ya mapema Jumanne, Vatican ilisema Papa alilala vyema usiku mzima na hivi sasa anaendelea vyema.

Francis alipatwa na matatizo hayo mawili siku ya Jumatatu. Madaktari waliondoa utandu mzito uliokuwa umekusanyika katika mapafu yake, Vatican ilisema katika taarifa mpya.

Walifanya vipimo viwili vya kuangalia mapafu na namna hewa inavyopita yaani Bronchoscopies ambapo bomba lililounganishwa na kamera lilipelekwa kwenye njia zake za hewa na kuvuta maji-maji yaliyokuwepo.

Papa huyo mwenye umri wa miaka 88 ambaye ana ugonjwa sugu wa mapafu na kwamba sehemu ya pafu lake moja liliondolewa akiwa kijana, alirudishwa kwenye kifaa cha upumuaji hewa ya ziada, akitumia barakoa inayofunika pua na mdomo wake na kusukuma oksijeni kwenye mapafu.

Forum

XS
SM
MD
LG