Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 11, 2024 Local time: 01:55

Shehena za misaada zawasili Lebanon


Mkazi wa eneo la kusini mwa Beirut akiwa amekaa njiani baada ya kujeruhiwa wakati wa shambulio la anga la Israel October 4, 2024.Picha na AFP
Mkazi wa eneo la kusini mwa Beirut akiwa amekaa njiani baada ya kujeruhiwa wakati wa shambulio la anga la Israel October 4, 2024.Picha na AFP

Msaada huo umetolewa siku moja baada ya mkurugenzi mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus kusema watashindwa kupeleka vifaa kwasababu ya masharti ya usafiri wa ndege.

Kaimu mwakilishi wa WHO nchini Lebanon, Dr Abdinasir Abubakar alisema shehena zaidi za misaada ya matibabu zinatarajiwa kuwasili katika siku zijazo.

Takriban wafanyakazi 28 wa huduma za afya wameuwawa katika saa 24 zilizopita huko Lebanon, ambako Israel ilianzisha mashambulizi ya anga na kutuma wanajeshi kupambana na kundi la wanamgambo la Hezbollah, Ghebreyesus alisema hayo alhamisi

Waziri wa Muda wa Afya wa Lebanon Firsa Abiad amesema “tuko hapa katika uwanja wa ndege wa Rafic Hariri mjini Beirut, kupokea vifaa ambavyo vimewasil hivi punde, ikiwemo vifaa vya matibabu na dawa kwa ajili ya majeruhi wa vita, vimeandaliwa na WHO na shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR, kwa msaada wa Umoja wa Falme za Kiarabu.”

Forum

XS
SM
MD
LG