Mamlaka zimesema waandamanaji walichoma moto kituo cha polisi, na gari la kutoa huduma za dharura kwenye kitongoji cha Dumbea, kilichoko kaskazini mwa mji mkuu wa Noumea, wakati ukumbi wa mji wa Koumac, uliopo karibu, pia ulichomwa moto.
Ghasia za karibuni zilitokea siku mbili zilizopita baada ya kiongozi anayeunga mkono uhuru Christian Tien na wanaharakati wengine 6 walipelekwa Ufaransa, ili kufunguliwa mashitaka ya kusababisha ghasia za awali zilizuka katikati mwezi Mei.
Ghasia hizo zimechochewa na mswaada uliokuwa katika bunge la Ufaransa,unao waruhusu wakazi wazaliwa wa Ufaransa ambao wameishi New Caledonia kwa miaka kumi, kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Viongozi wa harakati zinazounga mkono uhuru wa kisiwa hicho wamepinga hatua hiyo wakisema kuwa inapunguza nguvu ya upigaji kura ya wazawa wa kabila la Kanak, ambao wamebaguliwa kwa miongo mingi.
Forum