Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 14:21

Spika wa bunge la Afrika Kusini achukua likizo kufuatia tuhuma za rushwa


FILE PHOTO; Spika wa bunge la Afrika Kusini Nosiviwe Mapisa-Nqakula.
FILE PHOTO; Spika wa bunge la Afrika Kusini Nosiviwe Mapisa-Nqakula.

Spika wa Bunge la Afrika Kusini Nosiviwe Mapisa-Nqakula, alisema Alhamisi kwamba atachukua likizo maalum, kutokana na uchunguzi wa tuhuma za rushwa, wakati alipokuwa waziri wa ulinzi.

Wapelelezi walivamia nyumba ya Mapisa-Nqakula, siku ya Jumanne kama sehemu ya uchunguzi wa ufisadi, lakini hawakutoa maelezo zaidi kuhusu uchunguzi huo, au madai ya ufisadi.

Mapisa-Nqakula, ambaye alikuwa waziri wa ulinzi kutoka 2012 hadi 2021, amekana kufanya makosa yoyote.

"Kutokana na uzito wa tuhuma hizo na uvumi mkubwa wa vyombo vya habari, nimeamua kuchukua likizo maalum kutoka kwa nafasi yangu ya Spika wa Bunge, maera moja," Mapisa-Nqakula alisema katika taarifa yake.

Alisema hakuna taarifa rasmi ya hati ya kukamatwa kwake, au mawasiliano kuhusu kukamatwa kwake, kufuatia ripoti za vyombo vya habari vya ndani, kwamba alitarajiwa kujisalimisha kwa polisi siku ya Ijumaa.

Forum

XS
SM
MD
LG