Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 02:59

DRC: Umoja wa mataifa umetangaza vikwazo dhidi ya viongozi wa M23, FDLR na ADF


Waasi wa M23
Waasi wa M23

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limetangaza vikwazo dhidi ya viongozi sita wa makundi ya waasi wanaopigana mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Kati yao ni msemaji wa kundi la M23 Meja Willy Ngoma.

Wengine ni viongozi wa kundi la Allied democratic forces na FDLR wakiwiemo Apollinaire Hakizimana, Ahmad Mamood, Mikel Rukunda, Mohamed Ali Nkalubo, na William Amuri.

Vikwazo vinawazuia kupata silha, mafunzo, msaada wa kifedha na kusafiri

Taarifa ya baraza la usalama la umoja wa mataifa inasema kwamba Ngoma amelengwa kwa kuwa mmoja wa viongozi wa kisiasa na kijeshi wa kundi la waasi la M23 linaloshutumiwa kwa vita, mauaji na mateso ya raia mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Waasi wa M23 wanaoripotiwa kuungwa mkono na Rwanda wamekuwa wakipigana na wanajeshi wa DRC wakitaka kudhibithi mji wa Sake karibu na Goma.

Marekani ilimuwekea vikwazo Meja Willy Ngoma mnamo mwezi Desemba mwaka 2023 kutokana na mashambulizi na mauaji ya raia mashariki mwa Jmahuri ya kidemokrasia ya Congo.

Forum

XS
SM
MD
LG