Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 25, 2025 Local time: 10:03

Ghana: Watu sita wahukumiwa kifo kwa "kujaribu kupindua serikali"


Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo
Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo

Mahakama moja ya Ghana Jumatano iliwahukumu kifo watu sita, wakiwemo wanajeshi watatu wanaoshutumiwa kuhusika katika njama ya kupindua serikali ya nchi hiyo miaka mitatu iliyopita.

Watu hao walikamatwa mwaka wa 2021 walipokuwa wakifanya mazoezi ya silaha katika eneo la ufyatuaji risasi mjini Accra, na baadaye kwenda kwenye eneo ambapo waliamuru silaha hizo zikarabatiwe, kulingana na hati za mahakama.

Wote walikuwa wamekana mashtaka hayo wakati wa kesi hiyo. Idadi kubwa ya maafisa wa polisi waliojihami kwa silaha nzito nzito walionekana nje ya mahakama kuu, wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo na wakati hukumu ikitolewa.

Mmoja wa mawakili wa watu hao sita, Victor Adawudu, alisema timu ya utetezi itakata rufaa katika Mahakama ya Juu ya nchi hiyo, kupinga uamuzi huo. Mahakama kuu, hata hivyo, iliwaachilia huru afisa mkuu wa polisi Benjamin Agordzo, afisa wa jeshi Kanali Samuel Kodzo Gameli, na afisa mwingine wa ngazi ya chini katika jeshi, Koplo Seidu Abubakar.

Forum

XS
SM
MD
LG