Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 12, 2025 Local time: 08:09

Shambulizi mjini  Damascus, Syria laua maafisa waandamizi wanne wa Iran


Gari la mizigo likiinua gari lililoharibika karibu na eneo ambalo lilipigwa na shambulio la Israeli kulingana na vyanzo, katika kitongoji cha Mazzeh huko Damascus Syria Januari 20,2024. REUTERS.
Gari la mizigo likiinua gari lililoharibika karibu na eneo ambalo lilipigwa na shambulio la Israeli kulingana na vyanzo, katika kitongoji cha Mazzeh huko Damascus Syria Januari 20,2024. REUTERS.

Shambulio kwenye jengo la makazi mjini Damascus, Syria Jumamosi liliua askari wanne wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Iran ilisema ikiilaumu Israel.

IRGC ilithibitisha vifo hivyo katika taarifa kwenye vyombo vya habari vya Iran.

Mkuu wa Idara ya Upelelezi ya Walinzi wa Mapinduzi ya Syria, naibu wake na walinzi wengine wawili waliuwawa katika shambulio dhidi ya Syria na Israel, shirika la habari la Iran la Mehr lilisema likinukuu chanzo kinachofahamu habari hiyo.

Televisheni ya taifa ya Syria imesema jengo hilo ambalo liliharibiwa katika shambulio nyakati za asubuhi, lilikuwa katika kitongoji cha mji mkuu wa Syria ambako kuna balozi kadhaa.

Hakuna maoni ya mara moja kutoka kwa Israeli, ambayo ni mara chache inakubali hatua zake nchini Syria.

Forum

XS
SM
MD
LG