Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 02:43

Saba wakamatwa kupanga shambulizi la kigaidi Ubelgiji


Picha ya Maktaba
Picha ya Maktaba

Polisi wa Ubelgiji, Alhamisi wamewakamata watu saba wanaoshukiwa kulisaidia kundi la Islamic State, na njama ya shambulizi la kigaidi kwa mujibu wa waendesha mashitaka.

Takriban washukiwa wote ni watu wa kabila la chechnia, na watatu kati yao wana uraia wa Ubelgiji wamesema waendesha mashitaka katika taarifa.

Hata hivvyo haikuwekwa wazi ni wapi walikuwa wamepanga kufanya shambulizi hilo.

Polisi wakisaidiwa na vikosi maalumu walivamia nyumba tisa katika miji kaadhaa magharibu mwa Ubelgiji katika operesheni iliyo ongozwa na jaji wa uchunguzi ambaye amebobea katika kesi za ugaidi.

Jaji huyo ataamua katika hatua za baadaye kama kuna ushahidi wa kutosha kuwafungulia mashitaka washukiwa hao kwa mujibu wa taarifa.

Msemaji wa ofisi ya mwendesha mashitaka wa serekali kuu Eric Van Duyse, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba walikuwa wakitaka kulenga taasisi iliyopo Ubelgiji, na wamekuwa wakitafuta silaha.

Uvamizi wa polisi ulifanyika katika mji wa Ghent, na mIji mdogo ya Roeselare, Menen, Ostend, na Wevelgem.

XS
SM
MD
LG