Akiongea na wanahabari mjini Frankfurt, Ujerumani, Rais wa ECB, Christine Lagarde amesema wakati kiwango cha mfumuko wa bei kimeshuka kutoka kile cha juu cha zaidi ya asilimia 10 mwezi Oktoba, bado asilimia 7 inabaki kuwa cha juu sana.
Benki hiyo imesema viwango vilivyopita vyote ambavyo vilikuwa kati ya moja na nusu mpaka robo tatu ya poiniti ya asilimia, kinasambazwa kote katika sekta ya fedha ya muungano wao.
Bado haijawa wazi hata hivyo namna kinavyoweza kuathiri ya kiuhalisia kwa uchumi.