Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 23:54

Wademokrat karika Seneti ya Marekani waanzisha tena juhudi za kukabiliana na China


Wademokrat katika baraza la Senati Jumatano walizindua kuanzishwa tena kwa juhudi za kukabiliana na ushindani kutoka China.

Wanapanga sheria ya kuboresha uwezo wa Marekani kukabiliana na taifa hilo la Asia lenye nguvu katika masuala ya teknolojia mpaka usalama pamoja na vitisho kwa Taiwan.

Baada ya kupitisha mswaada wa jumla mwaka jana kukuza ushindani na Beijing katika vifaa vya umeme na teknolojia nyingine, kiongozi wa Demokrat katika Seneti, Chuck Schumer, na viongozi wa kamati za chama cha Demokrat, amesema wataandika mswaada na kutarajia kuuwasilisha katika kipindi cha miezi kadhaa ijayo.

Muswada huo ni kudhibiti mtiririko wa teknolojia kutoka China, kuizuia China kuzusha mgogoro na Taiwan, na kuweka kanuni kali kuzuia mitaji ya Marekani kwenda katika makampuni ya Kichina.

Schumer amesema anatarajia muswada utakubalika na pande zote, na kusema Warepablikan katika seneti wamekuwa wakiunga mkono mapendekezo ya mswaada.

XS
SM
MD
LG