Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 03, 2023 Local time: 19:16

Mauaji holela yaendelea nchini Haiti


Mauaji ya watu kiholela yanaongezeka katika mji mkuu wa Haiti na maeneo jirani ambapo wanaume watano waliuawa na kuchomwa moto Jumanne.

Kundi lililohusika liliacha moja ya miili karibu na kituo cha polisi cha eneo la watu matajiri.

Watu walionekana kutolewa wakiwa hai kutoka kwenye kitongoji duni cha Jalousie nje ya Port-au-Prince na kisha kuuawa kwa mujibu wa mashuhuda.

Maiti wengine waliachwa wakiwa wametapakaa kando ya barabara inayoelekea nyumbani kwa rais wa zamani Jovenel Moïse, ambaye aliuawa Julai 2021.

Mwili wa tano uliachwa karibu na kituo cha polisi katika kitongoji cha Petionville.

Ni jambo la kutisha kwa wao kuuawa mbele ya polisi, alisema Jean Marc Étienne, ambaye alishuhudia tukio hilo akiwa ameketi kwenye bustani mbele ya kituo cha polisi.

XS
SM
MD
LG