Katika Livetalk wiki hii tunajadili maadhimisho ya Siku ya watoto wa Mitaani tukiangazia mafanikio na changamoto zinazoendelea kukumba juhudi za kuboresha hali ya maisha ya watoto wapatao milioni 150 kote duniani ambayo inaelezwa kuathiriwa mno na kupanda kwa gharama ya maisha.