Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 23, 2024 Local time: 02:32

Manyanyanyaso ya kingono yanafanyika katika mashamba ya chai Kenya - BBC


Shamba la majani chai Kenya
Shamba la majani chai Kenya

Shirika la Utangazaji la BBC limesema Jumatatu limegundua ushahidi wa manyanyaso ya  kingono kwenye mashamba ya chai ya Kenya ambayo hupeleka  baadhi ya chapa maarufu za chai nchini Uingereza.

Katika video iliyobandikwa kwenye tovuti ya BBC World , msimamizi wa shamba la chai nchini Kenya alionekana akiwa na mwandishi wa habari wa siri aliyekuwa akifanya uchunguzi wa habari hiyo ambapo msimamizi huyo wa shamba alimuomba mwandishi huyo amguse na kumvua nguo, bila kufahamu alikuwa akirekodiwa na huku wafanyakazi wa BBC wakiwa jirani kwa ajili ya ulinzi wa mwandishi huyo wa habari.

Zaidi ya wanawake 70 waliiambia BBC kuwa wamekuwa wakinyanyaswa kingono na wasimamizi wao kwenye mashamba yanayomilikiwa na makampuni ya chai ya Unilever, Lipton na James Finlay & Co. Makampuni ambayo huuza badhi ya chapa maarufu sana nchini Uingereza, zikiwemo PG Tips na Lipton.

Baadhi ya wanawake waliiambia BBC kwamba hawakuwa na jinsi kwa sababau ya ukosefu wa ajira.

Katika shamba jingine, mwandishi huyo alihudhuria siku ya kutambulishwa kwa wafanyakazi wapya ambapo meneja alitoa hotuba iliyosema kampuni hiyo ilikuwa na sera ambazo hazivumilii unyanyasaji wa ngono.

Baadaye, meneja huyo alimkaribisha mwandishi huyo wakutane jioni katika baa ya hoteli hiyo na kupendekeza baadaye waende kwenye boma lake, BBC inaripoti.

XS
SM
MD
LG