Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 27, 2023 Local time: 15:51

Juhudi za uwokozi zaendelea Uturuki na Syria huku idadi ya vifo vikizidi 23 000


Idadi ya vifo kutokana na tetemeko la ardhi Uturuki na Syria imepindukia 11 000, huku matumaini ya kupata watu hai inapunguka
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:24 0:00

Idadi ya vifo kutokana na tetemeko la ardhi Uturuki na Syria imepindukia 23 000, huku matumaini ya kupata watu hai inapunguka

Juhudi za uwokozi kufuatia tetemeko kubwa la adhri nchini Uturuki na Syria zimeingia siku ya tano Ijuma kukiwa na matumaini madogo kabisa kuweza kupata watu zaidi hai, ingawa kumekuwepo na watu walookolewa kutoka baadhi ya miji.

Waokozi kutoka pende zote za dunia wamefika na wanashirikiana na wafanyakazi wa huduma za dharura wa Uturuki na Syria katika kazi za uwokozi.

Licha ya baridi kali na siku kuongezeka, watu zaidi waliokolewa Ijuma kutoka vifusi katika sehemu mbali mbali za Uturki.

Mjini Adiyaman mtu mwenye umri wa miaka 36 aliokolewa baada ya kua chini ya kifusi kwa saa 100. Mjini Diyarbakir mwanamke na vijana wake wawili waliokolewa wakati idadi ya walofariki imezidi elfu 23 katika nchi zote mbili Uturuki na Syria.

Waokozi wanatumia krani kumokoa Nur Bayraktar mjini Kahramanmaras, kusini mwa Uturuki.
Waokozi wanatumia krani kumokoa Nur Bayraktar mjini Kahramanmaras, kusini mwa Uturuki.

Sehmuz Cevik mfanyakazi wa uwokozi katika mji wa Diyarbakir anasema ni hisia ya aina yeke kuwezakumokoa hata mtu mmoja.

"Ni kitu cha ajabu. Ni kitu cha furaha. Tumekua tukifanya kazi bila ya kusita kwa siku tatu hapa. Tukapata mwanya mdogo katika kifusi. Na tukanaza kuuliza jee kuna mtu hapa, je kuna mtu huko. Halafu tukasikia sauti, hapo mimi nikadhani ninaota. Tunamshukuru mola."

Siku zinapoendea na baridi kuzidi, waatalamu wanasema hakuna uwezekano mkubwa wa kupatikana watu wengi hai.

Kwa upande mwengine hasira zinaongezeka miongoni mwa waathiriwa kuhusu namna serikali zao zimeshughulikia janga hilo.

Huko Syria mkuu wa huduma za dharura ya "White Helmet", Raed Al-Saleh ana utuhumu umoja wa mataifa kwa kutowasilisha msaada wa dharura unaostahiki katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi.

Nae Rais Bashar al-Assad wa Syria, akizungumza kwa mara ya kwanza baada ya janga kutokea na kutembelea hospitali ya Aleppo, na maeneo yaliyoharibika, amekosoa nchi za magharibi kuweka siasa mbele ya hali ya maisha ya binadam.

"Hawa hapa wanasema nchi za magharibi zimeipatia kipau mbele siasa kuliko hali ya binadam. Kupatia kipaumbele kitu kimoja kuliko kingine ni jambo la kawaida, hivyo hali ya kisiasa ni hali iliyopo, lakini hivi sasa maisha ya binadamu haionekani kua ni muhimu kwa nchi za magharibi. Kugeuza hali hii kua ya kisiasa sijambo zuri, inabidi kuzingatia hisia na mahitaji ya binadam kwanza." amesema Rais al-Assad.

Familia za waathiriwa wanendelea kua na hamu na kukata tamaa, wakisubiri kupata habari zaa ikiwa jamaa zao wako hai au mili yao itapatikana katika vifusi katika miji mbali mbali ya nchi hizi mbili.

Waokozi wanawatafuta wanusura katika kifusi kwenye mji wa Jableh nchini Syria
Waokozi wanawatafuta wanusura katika kifusi kwenye mji wa Jableh nchini Syria

Maelfu ya watu hivi sasa hawana makazi na hawajuli la kufanya Nihat Dag mkazi wa Hatay anasema hamombei mtu maafa kama haya.

"Mwnyezi mungu atusemehe simuombei mtu yeyote apitiye msiba kama huu na machungu haya. Tuna maelfu na maelfu ya walofariki. Huwenda idadi ya vifo ikafikia hata laki moja. Mugu asijaliye hivyo. Machungu yetu ni makubwa."

Wakati machungu na juhudi za kuwatafuta watu zinaendelea, waislamu katika matiafa yote duniani siku ya Ijuma wakati wasala wamewaombea kila la kheri Wa-turuki na Wa-Syria, na kuwasilia walofariki.

Hutba katika misikiti siku ya Ijuma ilizingatia zaidi janga hilo baya kuwahi kusabnabisha maafa makubwa namna hiyo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG