Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 20, 2023 Local time: 19:37

Papa Francis amewasili Sudan Kusini kwa ziara yake ya kwanza nchini humo


Papa Francis, Rais Salva Kiir, Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Welby na Msimamizi wa Kanisa la Scotland Lain Greenshields wakihudhuria mkutano na viongozi wa mashirika ya kiraia na mabalozi, katika Ikulu ya Rais,Juba, Sudan Kusini, Februari 3, 2023. REUTERS

Papa Francis amewasili nchini Sudan Kusini kwa ziara yake ya kwanza katika nchi changa sana duniani akikungana na mkuu wa Kanisa la England na Kanisa la Scotland kwa ziara ya Amani. Papa aliwasili siku moja baada ya afisa wa eneo kusema watu 27 wameuawa  katika ghasia za kijamii.

Papa Francis alipokelewa na maafisa wa juu wa Sudan Kusini kabla ya kuelekea kwenye makazi ya Rais Salva Kiir.

Kiongozi huyo wa wakatoliki takriban bilioni 1.4 mwenye umri wa miaka 86 atakutana na viongozi wa Sudan Kusini katika juhudi za amani na hali ya kibinadamu.

Francis alifuatana na mkuu wa Kanisa la England, Askofu wa Cantebury Justin Welby.

Wawili hao waliuangana na mkuu wa Kanisa la Scotland Mchungaji Lain Greenshields, ambaye aliwasili mjini Juba mapema siku hiyo.

Holy See ni wito wa kipekee katika ziara hiyo ambayo imetajwa na ‘hija ya amani’ nchini Sudan Kusini, nchi ambayo imeathiriwa na miaka mingi ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Viongozi watatu wa kanisa waliwasili siku moja tu baada ya afisa wa kieneo kusema watu 27 waliuawa katika ghasia za kijamii ambazo zilichochewa na wizi wa ng’ombe.

Mauaji yalifanyika katika moja ya kaunti huko Central Equatoria, mji mkuu wa utawala, Juba.

Katika Tweeti yake Welby alisema ‘ameshtutshwa’ sana na vifo, na kuita ni ‘hadithi ambayo mara nyingi inasikika nchini Sudan Kusini.’

Papa aliwasili kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, ambako alitumia muda wa siku kadhaa wiki hii, akiwaombea msamaha miongoni mwa pande zinazopigana,na kuitisha mkutano mkubwa wa vijana wa Congo.

Ziara ya Papa katika nchi hizo mbili ni sehemu ya juhudi za Vatican kujenga amani ya kudumu katika mataifa yaliyokumbwa na vita.

Amani imekuwa haiwezekani kwa Sudan Kusini tangu ijipatie uhuru kutoka Sudan mwaka 2011.

Wasudan Kusini wamekuwa wakisubiri kwa hamu kubwa ziara ya Papa tangu mwaka jana.

Francis alitarajiwa awali kuitembelea nchi hiyo Julai 2022 lakini ziara yake iliakhirishwa kutokana na tatizo la goti ambalo kwa kiasi kikubwa lilimfanya abakie kwenye kitu cha magurudumu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG