Tumeamua kumrudisha balozi wetu mjini Paris ili kufanya mashauriano kuhusu hali na mitazamo ya ushirikiano wetu baina ya nchi hizi mbili ilisema taarifa ya wizara hiyo.
Maandamano ya wapinzani juu ya kuwepo kwa jeshi la Ufaransa yameongezeka nchini Burkinafaso, ambayo kwa kiasi fulani yanahusishwa na dhana kwamba Ufaransa haijafanya vya kutosha kukabiliana na uasi wa Kiislamu ambao umeenea katika miaka ya hivi karibuni kutoka nchi jirani ya Mali.
Ufaransa siku ya Jumatano ilisema itaondoa wanajeshi wake mwezi ujao baada ya utawala wa kijeshi kulitaka kuondoka.