Mwalimu mmoja nchini Kenya aanzisha kampuni ambayom inatengeneza pikipiki zinazotumia nguvu za umeme kutoka kwenye betri za zamani za kompyuta za mkononi maarufu Laptop. Uvumbuzi huo, unatajwa kuwa njia nafuu na endelevu ya usafiri kwa kutumia rasilimali ambazo ni rahisi kupatikana.