Raia hao wawili Mustapha Jabbi na Saikuba Jabbi na Inspekta mdogo wa polisi Fakebba Jawara walikamatwa siku ya Ijumaa na kushtakiwa kwa uhaini na njama ya kutenda uhalifu.Waliwekwa rumande katika gereza la Mile 2.
Tarehe 21 Disemba, serikali ilisema ilizima jaribio la mapinduzi siku moja kabla na kuwakamata baadhi ya wanajeshi.
Mamlaka iliwakamata wanajeshi 7, akiwemo mmoja wa cheo cha kapteni na mwingine wa cheo cha Luteni.
Mwanasiasa wa upinzani Momodou Sabally, waziri wa zamani wa masuala ya urais chini ya kiongozi wa zamani Yahya Jammeh, alikamatwa na baadaye akaachiliwa.
Taifa hilo dogo la Afrika Magharibi wiki iliyopita liliunda jopo la kufanya uchunguzi kuhusu jaribio hilo la mapinduzi na lilipewa siku 30 kuwasilisha matokeo ya uchunguzi.