Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 14:34

Kampuni ya Shell italipa dola milioni 15.9 kwa jamii mbali mbali nchini Nigeria


Uzalishaji wa mafuta umechafua maji ya kunywa ya angalau jamii 10 katika eneo la Ogoniland Nigeria.
Uzalishaji wa mafuta umechafua maji ya kunywa ya angalau jamii 10 katika eneo la Ogoniland Nigeria.

Kampuni ya Shell italipa dola milioni 15.9 kwa jamii mbali mbali nchini Nigeria ambazo ziliathiriwa na kuvuja mafuta kutoka kwenye mabomba ya kampuni hiyo katika jimbo la Niger Delta.

Kampuni ya Shell italipa dola milioni 15.9 kwa jamii mbali mbali nchini Nigeria ambazo ziliathiriwa na kuvuja mafuta kutoka kwenye mabomba ya kampuni hiyo katika jimbo la Niger Delta, taarifa ya pamoja ya kampuni hiyo na kitengo cha Uholanzi cha Friends of the Earth.

Fidia ni matokeo ya mahakama ya Uholanzi iliyofikishwa mahakamani na Friends of the Earth, ambapo kampuni tanzu ya Shell nchini Nigeria ya SPDC mwaka jana iligundulika ilihusika na kumwagika mafuta na kuamriwa kuwalipa wakulima waliopata hasara.

Fedha hizo zitazinufaisha jamii za Oruma, Goi na Ikot Ada Udo nchini Nigeria, ambazo zimeathiriwa na umwagikaji mara nne wa mafuta uliotokea kat ya mwaka 2004 na 2007.

XS
SM
MD
LG