Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 01, 2022 Local time: 19:54

Mpalestina auwa Waisrael watatu katika ukingo wa magharibi


Eneo la tukio la shambulio la Novemba 15, 2022 katika Ukingo wa magharibi. Picha ya AFP

Maafisa wamesema leo Jumanne kwamba raia mmoja wa Palestina amewaua Waisraeli watatu katika Ukingo wa magharibi unaokaliwa, na kuchoma kisu vibaya wanaume wawili na kuwapiga kisu wengine kadhaa, kisha kumua mwingine kwa kutumia gari la wizi kabla ya kujiua mwenyewe kwa risasi.

Shambulio hilo baya limetokea saa chache kabla ya Israel kuapisha bunge lake jipya, huku wabunge wenye msimamo mkali wa mrengo wa kulia wakiwa tayari kuwa mawaziri, wakiapa kuwa watapambana na ghasia za Wapalestina.

Jeshi la Israel limeripoti shambulio la kisu karibu na eneo la viwanda la Ariel, kaskazini mwa Ukingo wa magharibi.

Taarifa ya jeshi la Israel imesema “Gaidi alifika kwenye mlango wa kuingilia eneo hilo na kuwachoma kisu raia katika eneo hilo.”

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG