Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 04, 2024 Local time: 02:39

Meli inayodaiwa kutaka kuiba mafuta ya Nigeria imekamatwa


Mitambo ya kuhifadhi mafuta mjini Lagos, Nigeria.
Mitambo ya kuhifadhi mafuta mjini Lagos, Nigeria.

Meli kubwa ya kubeba mafuta ambayo imeshutumiwa na serikali ya Nigeria kwa kujaribu kupakia mafuta ghafi kinyume cha sheria kabla ya kuondoka katika maji iya nchi hiyo, imelazimishwa kurudi ilipotoka.

Equitorial guinea iliikamata meli hiyo kwa jina Heroic Idun, kutokana na ombi la serikali ya Nigeria.

Idun ina uwezo wa kubeba mapipa milioni 2 ya mafuta, na ilikamatwa Agosti 17, kwa kusafiri bila bendera inayoitambulisha na hivyo ilikuwa vigumu kutambuliwa.

Ilikuwa inatokea katika maji ya Nigeria ikielekea Equitorial Guinea bila idhini.

Serikali ya Nigeria imesema kwamba meli hiyo inamilikiwa na kampuni ya Idun na msemaji wa jeshi la majini la Nigeria Commodore Kayode Ayo Vaughan, amesema kwamba meli mbili ndogo za jeshi la Nigeria, zinaisindikiza meli hiyo kurudi Nigeria.

Taarifa zinasema kwamba meli hiyo ilikuwa inaelekea Bonny, Nigeria. Makam rais wa Equitorial Guinea Teodoro Nguema Obiang, ameandika ujumbe wa twitter kwamba aliamuru meli hiyo kurudi Nigeria.

Nigeria hupoteza mapipa 400,000 ya mafuta kila siku kutokana na wizi.

XS
SM
MD
LG