Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 03:23

Waziri Blinken apongeza hatua ya kusitisha mapigano eneo la Tigray


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Lanseria mjini Johannesburg, Afrika Kusini, Agosti 7, 2022. Andrew Harnik /Pool kupitia REUTERS
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Lanseria mjini Johannesburg, Afrika Kusini, Agosti 7, 2022. Andrew Harnik /Pool kupitia REUTERS

Kufuatia makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya serikali ya Ethiopia na Tigray People’s Liberation Front-TPLF Waziri wa mambo ya nje wa Marekani amepokea vyema hatua hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya mambo ya nje ambayo VOA ilipata Waziri Anthony Blinken amesema "Tunakaribisha hatua muhimu iliyopigwa Pretoria hii leo kuendeleza kampeni ya Umoja wa Afrika ya "kunyamazisha bunduki" kwa kutia saini kusitishwa kwa uhasama kati ya Serikali ya Ethiopia na Chama cha Ukombozi cha Watu wa Tigray.

Katika taarifa yake ameongeza kusema kwamba “tunazipongeza pande zote kwa kuchukua hatua hii ya awali ya kukubaliana kusitisha mapigano na kuendelea na mazungumzo ili kutatua masuala ambayo hayajakamilika ili kuimarisha amani na kumaliza takriban miaka miwili ya migogoro.

"Tunakaribisha utoaji usiozuiliwa wa usaidizi wa kibinadamu na ulinzi wa raia ambao unapaswa kutokana na utekelezaji wa makubaliano haya." aliongeza.

"Marekani inampongeza Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika , Moussa Faki Mahamat kwa uongozi wake pamoja na juhudi za hali ya juu za Mwakilishi Mkuu wa AU Olusegon Obasanjo, Naibu Rais wa zamani wa Afrika Kusini Mlambo-Ngcuka, na Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta, ambao uwezeshaji wao ulisababisha hatua hii muhimu kuelekea amani. Pia tunaipongeza Afrika Kusini kwa kuandaa mazungumzo hayo kwa ukarimu." alisema.

Aliongeza kwamba "Marekani inasalia kuwa mshirika aliyejitolea kwa mchakato huu unaoongozwa na Umoja wa Afrika na kwa ushirikiano wetu na Umoja wa Mataifa, IGAD, na washirika wengine wa kikanda na kimataifa kusaidia utekelezaji wa makubaliano ya leo."

XS
SM
MD
LG