Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 19:05

Watafiti wanasema kupunguza ulaji wa nyama kutasaidia mazingira


Baba mtakatifu Francis aiwasili kusherekea misa huko Krakow, Poland Julai 31, 2016
Baba mtakatifu Francis aiwasili kusherekea misa huko Krakow, Poland Julai 31, 2016

Watafiti wanaeleza kuwa, iwapo Baba mtakatifu Francis, akiwahimiza wakatoliki kurejelea utamaduni wa kutokula nyama siku ya ijumaa, hio itaweza kusaidia kupunguza kiwango cha hewa chafu duniani.

Timu ya watafiti kutoka chuo kikuu cha Cambridge Uingereza, iliangazia athari ya wito uliotolewa na maaskofu wa Uingereza na Wales hapo mwaka 2011, wa kutaka waumini wao kurejea kwenye utamaduni wa kutokula nyama siku ya Ijumaa.
Watafiti waligundua kuwa licha ya idadi robo tu ya wakatoliki walibadili mienendo yao ya kula, hiyo ilichangia zaidi ya tani elfu 55 za hewa chafu kuokolewa kila mwaka.
Kwa kiwango cha kipimo cha hewa chafu, tani elfu 55 ni sawa kwa mfano wa watu takriban elfu 82 kutosafiri kwa ndege kutoka London hadi New York katika kipindi cha mwaka mmoja.
Watafiti wanaeleza kuwa iwapo dunia nzima itashirikishwa katika utamaduni wa kutokula nyama kila Ijumaa, hatua hiyo itasaidia mamilioni ya gesi ya hewa chafu kupungua kila mwaka.

Nyama ya ngombe ikiuzwa kwenye duka la Lambert's Rainbow Market mjini Westwood, Massachusetts, Juni 15, 2021
Nyama ya ngombe ikiuzwa kwenye duka la Lambert's Rainbow Market mjini Westwood, Massachusetts, Juni 15, 2021

Mwandishi Shaun Larcom kutoka idara ya uchumi wa ardhi kutoka chuo kikuu cha Cambridge, amesema kuwa kanisa katoliki lina nafasi nzuri katika kusaidia suala hili.
Anasema, iwapo Baba Mtakatifu Francis, atarudisha kuwawajibisha waumini wake duniani kote, kuto kula nyama kila ijumaa kutasaidia sana hatua hii ya kupunguza hewa chafu, hususan pia Baba mtakatifu Francis amesema kuwa mabadiliko ya hali ya hewa ni kitisho kikubwa ambacho hakijawahi kutokea, na kwamba hatua za haraka zinahitajika.

Ufugaji wa mifugo ni mojawapo ya vyanzo vikuu vinavyochangia hewa chafu.
Utamaduni wa kutokula nyama siku ya Ijumaa, mojawapo ya tamaduni za enzi nyingi, ambapo waumini wa kikristo walikula samaki badala ya nyama kama protini katika mlo wao.
Utamaduni huo haujawajibishwa kwa wakatoliki tangu mabadiliko ya Vatican ya miaka ya 60, ila kwa wakati wa Pasaka.
Watafiti wanaeleza kuwa utamaduni wa kutokula nyama siku ya Ijumaa, ulifuatwa sana na waumini wa kikatoliki Marekani, hatua iliyopelekea hata mgahawa maarufu wa Mc Donald’s Marekani, kuanza kuuza burger ya samaki.
Utafiti huo wa chuo cha Cambridge uliochapishwa kwenye mtandao wa Social Science Research, ulilenga juu ya masomo ya afya ya umma huko Uingereza na Wales.

Ripoti hii imetolewa na shirika la habari la AFP

XS
SM
MD
LG