Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 21, 2024 Local time: 21:30

Jinpin kuendelea kuongoza China kwa muhula wa tatu


Opening ceremony of Chinese Communist Party Congress
Opening ceremony of Chinese Communist Party Congress

Rais Jinpin wa China amesema katika hotuba ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa chama tawala cha Kikomunisti, awamu ya 20, mjini Beijing, kuwa China imeimarika kwa kasi na kuwa nchi yenye nguvu duniani . Jinpin alisema hayo bungeni ambapo wanachama wanatarajiwa kuidhinisha muhula wake wa tatu madarakani.

Naibu mkurugenzi wa tume ya maendeleo ya kitaifa Zhao Chenzin, amesema kwamba China itaimarisha juhudi zake za kuruhusu wawekezaji kutoka nchi nyingine kuwekeza nchini humo.

Amesema kwamba uwekezaji katika kampuni za China unaendelea kukua kwa kasi, na kwamba nchi hiyo imekabiliana vilivyo na changamoto kadhaa ikiwemo janga la kimataifa, hali mbaya ya kiuchumi duniani na mfumo dhaifu wa uwekezaji kati ya nchi.

XS
SM
MD
LG